Tarehe 30 mwezi wa kwanza mwaka 2012, ni siku tuliyopata mafunzo kuhusu matumizi ya Blogs kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Jijini Dar es salaam.
Mafunzo yalimefanyika katika kituo cha mafunzo cha "Tanzania global learning centre|"
na kuwezeshwa na mwandishi mshauri wa masuala wa mafunzo ya habari toka taasisi ya "the finnish foundation for media, and communication and develeopment-VIKES ya Nchini Finland, bw.Peik Johansson.
Katika mafunzo hayo tumejifunza mambo mengi kuhusu matumizi ya Mitandao,na namna mbavyo yanaweza kurahisisha kazi katika taaluma hii ya Habari.
Suala la haki miliki haki ni miongoni mwa mambo tuliyojifunza katika mafunzo hayo.
Tarehe 3 mwezi wa pili ni siku tuliyomaliza mafunzo ya siku tano kwa wahariri wa vyombo mbalimbali Jijini dar es salaam,
Tarehe 2,mwezi wa pili tulipata mwaliko toka kwa Ubalozi wa Finland hapa Nchini Balozi Sinikka Antila ambaye alitupa hamasa katika kuendeleza yote tuliyojifunza yaweze kutusaidia katika shughuli zetu za uandishi hasa katika masuala ya mawasiliano ya habari kupitia mitandao mbalimbali duniani.
Washiriki wengi wameweza kufungua mitandao yao, na kutuma mada mbalimbali.
Maggid Mjengwa ni mwezeshaji katika mafunzo hayo na pia ni mmiliki wa blog, na mwandishi wa makala mbalimbali, aliwasilisha mada kwa namna gani ameweza kuendesha mtandao wake na jinsi ya kuweka picha katika mtandao ilikuwa ni tarehe 3, mwezi wa pili siku ambayo tumehitimisha mafunzo hayo.
mafunzo yameandaliwa na Tasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania -MISA TAN na kufadhiliwa na Taasisi ya "the finnish foundation for media, and communication and develeopment-VIKES ya Nchini Finland.
washiriki kumi wamenufaika na mafunzo hayo.
TUNAWASHUKURU SANA, KWANI WENGI WETU TUMETOKA GIZANI!!!!!!
No comments:
Post a Comment